Rais Samia afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri, Bashungwa apelekwa Ulinzi, Dkt.Tax apelekwa Mambo ya Nje, Kairuki apelekwa OR-TAMISEMI

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 2, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Katika uteuzi huo, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Pili,Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Tatu, Mheshimiwa Rais amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa Oktoba 3, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news