Rais Samia afanya uteuzi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Polisi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 24, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, pia Mheshimiwa Rais Samia amemteua Kamishna Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Raslimali watu wa Jeshi la Polisi.

Post a Comment

0 Comments