Rais Samia ampa kongole Rais Xi Jinping

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amempongeza Rais wa China Xi Jinping, kwa kuchaguliwa tena kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Mheshimiwa Rais Samia ametoa pongezi hizo leo Oktoba 24, 2022 baada ya Rais Xi Jinping kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa kamati hiyo.

Ni kupitia Mkutano Mkuu wa 20 wa chama tawala cha China Chama cha Kikomunisti cha China CPC uliofanyika kwa siku saba kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
"Pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa China Xi Jinping, kwa kuchaguliwa tena kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),"amesema Mheshimiwa Rais Samia.

Aidha, mkutano huo ulichagua Kamati Kuu ya 20 ya CPC na Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu, kupitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC.

Sambamba na kupitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati Kuu ya 19 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, na azimio kuhusu marekebisho ya Katiba ya CPC.

Mkutano mkuu wa CPC na kamati kuu iliyochaguliwa na mkutano huo ni vyombo vikuu vya uongozi vya CPC ambapo Mkutano Mkuu wa CPC unafanyika kila baada ya miaka mitano.

Rais Xi Jinping kupitia hotuba yake amesema, kuanzia sasa jukumu kuu la chama hicho ni kuongoza wananchi wa makabila mbalimbali nchini humo.

Pia kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa katika pande zote, na kutimiza lengo la pili la miaka 100 ili kusukuma mbele ustawishaji wa taifa la China kwa njia ya China .

Amesema, China inafuata sera za diplomasia ya amani ya kujitawala na kujiamulia na siku zote Taifa hilo linaamua msimamo na sera zake kufuatia hali halisi, kulinda kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa na haki duniani.

Aidha, China inapinga aina yoyote ya siasa za kimabavu ikiwemo wazo la Vita Baridi, vitendo vya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Amesema, China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa nchi na sehemu zaidi ya 140 duniani, na inashika nafasi ya kwanza duniani kwa thamani ya biashara ya bidhaa. 

Raia Xi amesema,Taifa hilo linashika nafasi ya kwanza katika kuvutia uwekezaji wa nje na kutoa uwekezaji kwa nchi za nje, na imeendeleza sera ya kufungua mlango kwa nje kwa upana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news