RAIS SAMIA KUPOKEA NA KUZINDUA RASMI CHUO CHA VETA KAGERA

NA MWANDISHI WETU, WyEST

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania anatarajiwa kupokea na kuzindua Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera.
Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika AlhamisI tarehe 13 Oktoba, 2022 katika chuo hicho kipya kilichopo Burugo Nyakato Kagera.

Chuo hicho chenye karakana, vifaa na miundombinu ya kisasa kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya China, kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1,400 kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika fani mbalimbali za ufundi na huduma.
Hayo yameelezwa na Prof. Adolf Mkenda ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokagua maandilizi ya hafla hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wa Mkoa wa kagera na mikoa mingine ya jirani kushiriki katika ufunguzi huo.Ametumia nafasi hiyo pia kuwataka vijana kujiunga na mafunzo ambayo yanalenga katika kujenga ujuzi yatakayokuwa yanatolewa katika chuo hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news