Serikali yatoa wito kwa wadau kuhusu maafa

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga amewahimiza wadau wa maendeleo na watu binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kuchangia vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akikagua ghala la kuhifadhi vifaa vya msaada wakati wa maafa lililopo mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Ummy ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua ghala la kuhifadhi vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa Kanda ya Kaskazini lililopo maeneo ya Chekereni, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.

Amesema, uungwaji mkono wa serikali kutoka kwa wadau unasadia wananchi kufikiwa na huduma kwa haraka kutokana na majanga yaliyojitokeza ambayo husabababisha madhara kama vifo, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika pamoja na miundombinu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati alipotembelea na kukagua ghala la kuhifadhi vifaa vya msaada wa kibinadamu wakati wa maafa lililopo mkoani Kilimanjaro.

“Nitoe wito kwa wadau na watu mbalimbali ambao wanaguswa kushirikiana na serikali kwa kutoa vifaa wafanye hivyo pengine ngaji ya Wilaya, Mkoa na hata kijiji ili tuwe navyo vya kutosha ili yanapotokea tunatoa msaada kwa haraka,”amehimiza Mhe. Ummy.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (aliyeinama) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu (kulia).

Pia Mhe. Ummy alisisitiza utunzwaji wa magahala hayo hatua itakayosaidia vifaa hivyo kudumu kwa muda mrefu na kuwa tayari kutumika pindi vinapohitajika katika maeneo yenye maafa.
Afisa Ugavi Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro,Bw.Claude Kilala akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Ummy Nderiananga alipotembelea ghala hilo. 

Aidha, ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa utayari wa kutoa msaada wa kibinadamu kwa wananchi wanaokumbwa na maafa kwa lengo la kuwasaidia kurejea katika hali yao ya awali.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe.Ummy Nderiananga (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa huo. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni Afisa Mifugo katika Mkoa huo Bwa. James Shao alisema ghala la Kanda ya Kasikazini linahudumia mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news