Rushwa ya ngono yawatesa wanahabari

NA DIRAMAKINI

RIPOTI ya Haki za Binadamu na Biashara ya mwaka 2021/2022 iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam imeonesha kuwa, rushwa ya ngono kwa waandishi wa habari wanawake ni janga kubwa linalowakawamisha katika tasnia hiyo nchini.

Bi.Joyce Komanya ambaye ni Afisa Programu Mwandamizi Masuala Biashara na Haki za Binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) alisema, asilimia ya wanawake waliohojiwa walisema hali ya rushwa ya ngono ni mbaya.

Alisema, wengine asilimia 40 walisema ni mbaya lakini kawaida, asilimia 4 walisema ni mbaya na waliwahi kushuhudia na asilimia zaidi ya 10 walisema hawajui.

Bi.Komanya alisema, changamoto kubwa ambayo waandishi wa habari wanawake waliielezea walisema ni rushwa ya ngono na walivyozungumzia rushwa ya ngono waliwauliza hiyo changamoto ni, "kubwa kiasi gani,ni mbaya sana, ni mbaya kiasi, ni kawaida au hakuna kabisa,"alisema.

Afisa huyo alifafanua kuwa, rushwa ya ngono ina athari kimwili, kiakili huku akitolea mfano mfanyakazi anayekwenda ofisini kila siku na mkubwa wake kazi anamfanyia matendo hayo hawezi kufanya kazi vizuri hivyo hata utendaji kazi unaathirika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news