SDF waneemesha mamia ya vijana,wanawake mkoani Mbeya

NA MWANDISHI WETU

MAFUNZO ya Kuendeleza Ujuzi yanayotolewa kupitia ruzuku ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) yametengeneza fursa za ajira kwa mamia ya vijana na akinamama katika wilaya ya Rungwe jijini Mbeya kupitia mradi wa kufuga samaki.
Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia (WB), Bi. Innocent Mulindwa (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara katika Kampuni ya RiversBank Fish Farm Wilayani Rungwe.

Mkurugenzi wa shamba la kufugia samaki la RiversBank Fish Farm, Pius Nyambancha ambalo ni miongoni mwa taasisi zilizofadhiliwa na SDF amebainisha hayo alipozungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na wawakilishi wa Benki ya Dunia (WB) ambao ni wafadhili wa Mradi huo wa Kuendeleza Ujuzi (SDF).

Amesema, ruzuku ya SDF imemwezesha kufuga samaki kitaalam ikiwa ni pamoja na kumpa uwezo wa kuzalisha vifaranga hivyo kumwongezea uzalishaji ambapo katika kipindi cha miezi tisa amezalisha kilo 600 za samaki na hivyo kujiongezea kipato.
Mkurugenzi wa Kampuni ya RiversBank Fish Farm,Pius Nyambacha (mwenye kofia) akifurahia jambo na ujumbe uliofanya ziara katika mashamba yake ya kufugia samaki.

Kupitia ruzuku ya SDF, Kampuni ya RiversBank Fish Farm ilipata ufadhili wa Shs. Milioni 131.2 ambazo zimewezesha uboreshaji wa miundombinu ya uzalishaji vifaranga vya samaki, ufugaji wa kisasa, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya ufugaji pamoja na kuendesha mafunzo kwa vijana na akina mama 427 Wilayani Rungwe.

Nyambacha ameongeza kuwa, baada ya kujengewa uwezo na SDF amefanikiwa kutengeneza ajira kwa watanzania 726.
Wajumbe kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Mamlaka ya Elimu Tanzania na Benki ya Dunia (WB) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya RiversBank Fish Farm.
Ujumbe kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, TEA na Benki ya Dunia (WB) uko mkoani Mbeya kwa ziara ya siku nne ya ukaguzi wa miradi katika taasisi zilizonufaika na ufadhili wa SDF.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news