SERIKALI YAOMBA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imetoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kuhimiza jamii kuepuka uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya na kujenga uelewa kuhusu madhara ya dawa za kulevya.
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Musabila (Kulia) katika picha wakati wa kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/23.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya jijini Dodoma.

“Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za kulevya, itaendelea kushirikiana na Wizara nyingine katika kuona namna nzuri ya kuandaa maudhui ya mtandaoni ili kuelimisha vijana kuhusu athari ya dawa za kulevya kama ambavyo Tume ya Kudhibiti UKIMWI inavyofanya”.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya alipokuwa akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/23.

"Tupo kwenye utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imetoa maelekezo mahususi kuhusu kushughulikia dawa za kulevya,"amesema Naibu Waziri.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya,Dkt. Alice Karungi ameipongeza serikali kwa kiwango cha fedha kilichopelekwa kwenye Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kinachoendana na kwa kiwango cha fedha kilichokadiriwa wakati wa bajeti.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Dkt. Alice Karungi akizungumza wakati wa kupokea taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/23.

“Zoezi la kuwasaidia vijana wetu waliopata nafuu ya uraibu wa dawa za kulevya kwa kupatiwa mafunzo ya kukuza ujuzi; kama sehemu ya jitihada za Mamlaka, katika kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, liwe endelevu”.

Naye Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Musabila amesema mamlaka imeweka msukumo mkubwa katika kukabiliana dawa zinazotoka nje ya nchi, Heroin, Cocaine na Methamphetamine.

“Bangi imekuwa ikitumika kwa wingi kwa sababu inapatikana kwa bei nafuu na zinalimwa katika maeneo ya kujificha sana”.

"Tamaa ya kupata fedha imekuwa ikichochea wananchi kulima bangi kulinganisha na mazao mengine hata hivyo udhibiti unaendelea.
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za Kulevya Mhe. Neema Mwandabila akizungumza jambo wakati wa kupokea taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/23 kwa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu.(Picha na OWM).

“Tunashirikiana na wenzetu wa Wizara ya Klimo waweze kushauri Mwananchi badala ya kulima bangi walime zao gani ambalo litawasaidia kupata fedha nyingi.”

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Dkt. Leonard Maboko ameihakikishia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya kwamba fedha za Global Fund zitatoka robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/23.

“Mradi wa Umoja wa Mataifa wa Kuhusisha UKIMWI kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa katika bajeti 2022/23 iliyoidhinishwa ya shilingi 2,132,610,000.00, tayari kiasi cha shilingi 1,090,849,597.00 zimepokelewa. Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) katika bajeti 2022/23 iliyoidhinishwa ya shilingi 1,880,000,000.00 fedha za ndani, tayari kiasi cha shilingi 469,992,000.00 zimepokelewa mwishoni mwa mwezi Septemba 2022 hivyo zitatumika katika robo ya pili ya mwaka (Oktoba – Desemba, 2022)”.

Naye Mhe. Asia Halamga ameomba serikali kubadili baadhi ya Sheria zinazowazuia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya iweze kufanya kazi zake kikamilifu.

“Fedha tunazotumia kutibu ni vyema tukazitumia kudhibiti ili tusiendelee kuumiza taifa na hasa vijana”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news