Tanzania, Zambia zajadiliana maeneo ya ushirikiano

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia zinakutana jijini Lusaka, Zambia kujadili masuala ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya nchi hizo mbili.

Balozi wa Tanzania nchini Zambia anayemaliza muda wake, Mhe. Hassan Simba Yahya akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kumi wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia - Ngazi ya Wataalam unaofanyika leo tarehe 11 Oktoba 2022 jijini Lusaka Zambia.

Majadiliano hayo yanafanyika katika ngazi ya Wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Kumi wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia unaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 14 Oktoba 2022.

Mkutano wa Wataalam utafuatiwa na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 12 Oktoba 2022 na kumalizika na mkutano ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 14 Oktoba 2022 jijini Lusaka Zambia.

Mkutano huu unajadili na kutathimini utekelezaji wa maazimio katika sekta mbalimbali za ushirikiano zilizokubaliwa katika mkutano wa tisa uliofanyika tarehe 25 hadi 26 Februari 2016 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Maeneo ya ushirikiano ni pamoja na; Siasa, Ulinzi na Usalama, Mambo ya Nje, Uhamiaji, Fedha na Uchumi, Sheria, Nishati, Habari na Mawasiliano, Kilimo, Miundombinu, Uchukuzi na Usafirishaji, Elimu, Sayansi na Teknolojia, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Utalii, Kilimo, Uvuvi, Mazingira na Maliaasili, Afya, Elimu, Vijana na Michezo na jinsia.

Mkutano huu unafanyika kufuatia maagizo ya Marais wa pande zote mbili wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Zambia nchini Tanzania, Mhe. Hakainde Hichilema mapema mwezi Agosti 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news