TAKUKURU YATAKIWA KUFANYA UCHUNGUZI WA MATUMIZI YA FEDHA ZA TASAF ZILIZOTOLEWA KUJENGA ZAHANATI

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amemtaka Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Ruangwa kufanya uchunguzi wa matumizi ya kiasi cha shilingi milioni 102,080,357.14 zilizotolewa na Serikali kupitia TASAF ili kujenga zahanati katika Kijiji cha Mtakuja wilayani Ruangwa na kuwasilisha taarifa ya uchunguzi huo kwake kabla ya kuhitimisha ziara yake mkoani Lindi.

Post a Comment

0 Comments