TANZIA:Mbunge afariki

NA DIRAMAKINI

MBUNGE wa Jimbo la Amani lililopo Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Mussa Hassan Mussa, amefariki dunia leo jijini Zanzibar.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson.

Aidha, Mheshimiwa Spika ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge pamoja na wananchi wa jimbo la Amani kufuatia msiba huo. 

Kwa mujibu wa taarifa mwili wa marehemu unapelekwa kijijini kwao Bwejuu  kwa ajili ya maziko yanatarajiwa kufanyika saa kumi leo baada ya sala ya alasiri. 

Innalillahi waina ilaihi rajiun Allah amsameh makosa yake na awape subra wafiwa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news