TCU yaongeza muda wa udahili

NA GODFREY NNKO

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa, udahili katika awamu zote tatu kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2022/2023 umekamilika kwa mujibu wa ratiba ya udahili.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 3, 2022 kupitia taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Dkt. Kokuberwa Katunzi-Mollel huku akifafanua kuwa, majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Tatu yanatangazwa na vyuo husika.

Kwa mujibu wa Dkt.Mollel waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Tatu na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita wanahimizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo Oktoba 3 hadi 24 Oktoba, 2022 kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.

"Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

"Uthibitisho wa udahili unafanyika kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili. Orodha ya majina ya waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja imewekwa kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).

Awamu ya nne

Dkt.Mollel amefafanua kuwa,baada ya kukamilika kwa awamu zote tatu za udahili, tume imepokea maombi ya kuomba kuongezwa muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili.

"Hivyo,tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Nne na ya mwisho ya udahili inayoanza leo tarehe 3 hadi 07 Oktoba, 2022. Tume inasisitiza kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakufanikiwa kudahiliwa katika awamu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma kwa usahihi maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.

"Tume inaelekeza taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazofanya udahili wa Shahada ya Kwanza kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi,"amefafanua Dkt.Mollel.

Utaratibu

Amesema, waombaji wa udahili na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa Awamu ya Nne kama ilivyoainishwa hapa chini;

Utaratibu wa udahili katika Awamu ya Nne kwa mwaka wa
masomo 2022/2023
"Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

"Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa. TCU inawaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini,"amefafanua Dkt.Mollel.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news