TUOMBE KWA UNYENYEKEVU ASEMA PADRI MREMA

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa kila wanapokwenda kanisani wanaabudu, wanasali,wanasikiliza neno la Mungu na kuomba msamaha ili kupata neema ya Mungu na vile vile wanakwenda kufahamu mambo yanayompendeza Mungu, kumshukuru Mungu kwa yale mema anayotenda katika maisha yetu yao.
Hayo yamesemwa na Padri Novatus Mrema, Paroko wa Parokia ya Mbagala Kizuiani, Kanisa wa Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakati wa misa ya kwanza ya Jumapili ya 30 ya mwaka C, Oktoba 23, 2022.

Akiendelea kuhubiri Padri Mrema amesema kuwa, kila mara mkristo anapokwenda kusali anahimizwa na masomo ya jumapili hii juu ya toba.
“Je sala zako zinafanana na ya mfarisayo au zinafanana na ya mtoza ushuru? Mfano huo ni sawa na kioo kilicho mbele yetu, ili tuweze kujiona.”

Ameongeza kuwa, si vizuri kujiona wewe ni mwenye haki zaidi ya mwingine, mbele ya Mungu tuyaone madhaifu yetu na kujinyenyekeza.

Misa hiyo pia ilikuwa na maombi kadhaa likiwamo ombi hili,“Eee Baba Mungu sisi ni kama mtoza ushuru, hatuna kitu mbele yako, usikilize sala zetu katika unyenyekevu tunaokutolea kila siku.”
Kwa juma zima hali ya hewa ya Jiji la Dar es Salaam ilikuwa ya jua kiasi, lakini hali hiyo ilibadilika kwa siku ya Jumamosi ya Oktoba 22, 2022 katika baadhi ya maeneo ambapo kulikuwa na mvua iliyonyesha na kuacha madimbiwi ya maji kutuama katika baadhi ya mitaa ya jiji hili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news