Waliovamiwa na 'Panya Road' watuma salamu maalumu kwa IJP Wambura

NA DIRAMAKINI

WAKAZI wa Buguruni Kisiwani, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaa wametuma salamu maalumu kwa Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkuu wa Jeshi hilo, IJP Camillius Wambura wakimtaka aendelee na operesheni za kuwakabili wahalifu hususani Panya Road, ambao wamekua wakihatarisha usalama wa maisha yao.
Wananchi hao wamesema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi GANA ambapo walitoa maoni yao kuhusiana na namna Jeshi la Polisi walivyojitoa kupambana na Panya Road na kutumia muda huo kutuma salamu maalum kwa IJP Wambura.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto amewaambia sababu kubwa ya kuwepo Panya Road ni wazazi kutowasihi watoto wao kusoma licha ya jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye utoaji wa elimu bure, hivyo amewataka kumuunga mkono Rais Samia kuitikia wito wake wa kuwapeleka shule watoto.

Post a Comment

0 Comments