Watanzania waazimia kuvunja rekodi Mashindano ya Urembo, Utanashati na Mitindo ya Dunia kwa Viziwi jijini Dar

NA ADELADIUS MAKGWEGA-WUSM

WAKUFUNZI wanaofundisha miondoko kwa washiriki wa Tanzania katika kambi inayojiandaa na Mashindano ya Urembo, Utanashati na Mitindo ya Dunia yatakayofanyika Oktoba 29, 2022 jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kwa sasa washiriki wote wako vizuri wana ari ya kushiriki na kushinda mashindano hayo.
Haya yamesemwa kwa pamoja na wakufunzi Nasra Swalehe na John Mushi katika kambi hiyo iliyopo Hoteli ya Peacock Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

“Maandalizi ni mazuri, washiriki wanaendelea vizuri, mpaka sasa Watanzania na vijana wenzetu wako na ari ya ushindi, wanajitoa kwa moyo wote kupambania wito wao, kuliwakilisha vema taifa letu".
Jambo hili limetutia moyo mkubwa na tunahimiza pia kila vijana wa taifa letu wanapopata nafasi ya kutuwakilisha popote pale wajitoa kwa moyo wote na ushindi wao ni wa kila Mtanzania. Vijana wajitokeze kwa wingi kila mashindano kama haya yanapotangazwa,kwani sasa ulemavu siyo kikwazo,"amesema mkufunzi Nasra Swalehe ambaye aliwahi kuwa Mshindi wa Miss Dar es Salaam mwaka 2021/2022.

Kwa upande wake mkufunzi wa miondoko John Mushi ametoa ahadi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na kwa Watanzania wote kuwa ushindi Oktoba 29,2022 ni wetu kwa kuwa viwango vya washiriki vipo juu.
Mshiriki mmojawapo wa Tanzania Mashindano ya Urembo, Utanashati na Mitindo ya Dunia, Oktoba 29, 2022 jijini Dar es Salaam,Russo Songoro mwenye umri wangu wa miaka 25 mkazi wa Shinyanga amesema anatarajia kufanya makubwa.

"Elimu ya msingi nimesoma Buguruni Viziwi 2002-2011 na sekondari nimesoma huko Kilifi Mombasa nchini Kenya.Ujuzi wangu ni upishi niliyosomea hapo Cefa-Mikocheni (B) jijini Dar es Salaam.Ninapenda mitindo, utanashati, kucheza mpira wa miguu na kucheza muziki.Ahadi yangu kwa Watanzania ni kushinda na kuwa balozi mzuri kwa jamii ya viziwi na Watanzania wote,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news