Waziri Mchengerwa aipa tano Serengeti Girls kwa kuibamiza Ufaransa

NA JOHN MAPEPELE

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Soka ya Wanawake Serengeti Girls kwa kuibamiza timu ya Ufaransa mabao 2-1 katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini India.

Magoli ya Tanzania yamefungwa na Diana Mnaly na Christer Bahela.

Waziri Mchengerwa amesema, wachezaji wameonesha uzalendo mkubwa kwa nchi yao na amewataka kuendelea kucheza kufa na kupona katika mechi zilizosalia ili kurejesha kombe nyumbani.

Aidha, amesisitiza kuwa Serikali ipo pamoja na timu hiyo katika kila hatua ili kuhakikisha inarudi na kombe nchini.

Amewaomba watanzania kwa umoja wao waiombee timu hiyo ili hatimaye ishinde mechi zilizobaki na kutwaa kombe.

Kwa matokeo hayo Tanzania inashika nafasi ya pili nyuma ya Japan na nafasi ya tatu Canada na nne ni Ufaransa, huku ikiwa na mechi moja mkononi dhidi ya Canada itakayochezwa Oktoba 18, 2022 jijini Mumbai, India.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news