BRELA, ARIPO watembelea mawakala Dar

NA MWANDISHI WETU

MAAFISA Waandamizi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), kwa kushirikiana na Maafisa Waandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) leo Novemba 10, 2022 wamefanya ziara ya kutembelea mawakala sita wa Tanzania waliopo jijini Dar es Salaam.
Lengo ni kuona namna ambavyo wanasajili alama za biashara, huduma pamoja na kutoa hataza kwa wafanyabiashara na wavumbuzi wa Tanzania kupitia mfumo unaosimamiwa na ARIPO na kusikiliza changamoto wanazopitia mawakala hao pindi wanaposajili kupitia mfumo.

BRELA inaendelea kuhamasisha wafanyabiashara kusajili Alama za Biashara na Huduma pamoja na kupata Hataza ili kupewe ulinzi wa Kisheria. Mawakala waliotembelewa ni Bowmans Tanzania, AKP Laws Advocates, FB Attorneys, NexLaw, Lexglobe IP Services na Crystal Associates.
Pichani ni Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) leo Novemba 10, 2022 wakiwa na Mawakala kutoka kampuni sita za jijini Dar es Salaam, zinazotoa usaidizi wa Usajili wa Alama ya Biashara na Huduma pamoja na utoaji wa Hataza kwa wafanyabiashara na wavumbuzi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news