Chama,Aziz Ki wafungiwa mechi tatu kwa makosa yanayofanana

NA DIRAMAKINI

VIUNGO washambuliaji, Mzambia Clatous Chota Chama wa Simba na Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso wamefungiwa mechi tatu kila mmoja kwa makosa yanayofanana.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 8, 2022 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Adhabu hiyo imetolewa, baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligii Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Novemba 4, 2022 kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi.

Imeelezwa kuwa, katika mechi Namba 64 ambayo iliwakutanisha Yanga SC na Simba SC katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Oktoba 23, 2022 walikwepa kusalimiana.

"Mchezaji wa timu ya Young Africans, Stephan Aziz Ki na Clatous Chama wa Klabu ya Simba wamefuniwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi 500,000 kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo huo,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, adhabu hiyo ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 41:5 (5.4) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa wachezaji.

Post a Comment

0 Comments