Yanga SC yapigwa faini milioni 5/- kwa kutumia mlango usio rasmi

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imetozwa faini ya shilingi milioni 5 kwa kosa la kuingia chumba cha kuvalia kupitia mlango usio rasmi.

Ni katika mechi Namba 64 ambayo iliwakutanisha Yanga SC na Simba SC katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Oktoba 23, 2022.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 8, 2022 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Adhabu hiyo imetolewa, baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligii Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Novemba 4, 2022 kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi.

"Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 17: (21 na 60) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments