Dunia yaelekeza macho na masikio Bagamoyo katika Tamasha la Kimataifa la 41 la Utamaduni na Sanaa

NA JOHN MAPEPELE

TAMASHA la Kimataifa la 41 la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo linaanza leo Novemba 10, 2022 mjini Bagamoyo mkoani Pwani kwa kufanya kongamano itakalojadili kwa kina masuala ya sanaa na uchumi litalaloongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Wadau mbalimbali wa sanaa kutoka ndani na nje ya nchi na watendaji wakuu wa makampuni makubwa nchini wamealikwa kuchangia katika mdahalo huo.
Aidha, baada ya kongamano hilo, kutakuwa na maonesho ya kazi za sanaa kwenye viwanja vya Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) na usiku kupambwa na tumbuizo la michezo mbalimbali ya sanaa ambapo vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka maeneo mbalimbali duniani vitapamba.
Kesho, ambayo ni siku ya pili ya Tamasha, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, Philipo Mpango atafungua rasmi tamasha hilo ambapo usiku vikundi mbalimbali vitatumbuiza na Mgeni maalum katika usiku huo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Siku ya mwisho, tamasha litatamatishwa na burudani kali kutoka kwa wasanii mbimbali ambapo Mgeni maalum atakuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul.
Aidha, siku ya mwisho washiriki wote watapata fursa ya kufanya Royal Tour ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika mji wa Bagamoyo na kutembelea kisiwa cha Liz lagoon.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news