Ecuador yaichapa Qatar mabao 2-0 michuano ya Kombe la Dunia 2022

NA DIRAMAKINI

TIMU ya Taifa ya Ecuador imekuwa ya kwanza kujizolea alama tatu zikisindikizwa na mabao mawili katika michuano ya Kombe la Dunia 2022 inayoendelea nchini Qatar.

Ni baada ya kuwapiga mabao mawili wenyeji Qatar, Novemba 20, 2022 kupitia mtanange wa moto naa wa ufunguzi uliopigwa katika Dimba la Al Bayt Stadium lililopo Al Khor, Qatar.

Mshambulizi wa Fenerbahce, Enner Valencia aliifungia Ecuador bao la mapema dakika ya tatu kabla ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR) kulikataa.

Valencia aliweka mpira tena langoni mwa Qatar, kwa mkwaju wa penalti, dakika ya 16, na kisha dakika ya 31, akafunga tena kwa kichwa.

Aidha, licha ya uchezaji bora wa Qatar baada ya bao la pili la Ecuador na Almoez Ali kukosa mkwaju muhimu katika sekunde za mwisho. Pedro wa Qatar alipoteza nafasi nyingine muhimu ya bao dakika ya 61. Baada ya shuti la mbali la Muntari wa Qatar kuzikosa nyavu za Ecuador kwa dakika ya 85, mchezo ulimalizika kwa Ecuador kwa mabao 2-0.

Kutokana na matokeo haya, Qatar imekuwa wenyeji wa kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kupoteza mechi ya ufunguzi.

Ecuador sasa inaongoza Kundi A la Kombe la Dunia kwa alama tatau huku Qatar ikishika nafasi ya nne kwa sifuri.Senegal itamenyana na Uholanzi katika mechi inayofuata ya Kundi A leo Novemba 21, 2022.

Post a Comment

0 Comments