Jeshi la Zimamoto na Uokoaji latekeleza mara moja maagizo ya Rais Samia kuhusu kijana Majaliwa Jackson Samweli

NA GODFREY NNKO

MKUU wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali John Masunga amesema, tayari Majaliwa Jackson Samweli amepokelewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Majaliwa Jackson Samweli akiwa ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kagera akipokelewa na Kamanda wa Mkoa kamishna msaidizi mwandamizi Zablon Muhumha.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji makao makuu jijini Dodoma, SACF Puyo Nzalayaimisi ikiwa ni saa chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutoa maagizo hayo.

Novemba 7, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameagiza kijana Majaliwa Jackson Samweli aliyeona ndege ikianguka na kuamua kwenda kutoa msaada wa uokoaji akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na aingizwe katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili apate mafunzo zaidi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyasema hayo wakati akiongoza wananchi kuaga miili ya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya shirika la ndege la Precision Air katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Ajali ya ndege hiyo aina ya ATR 42-500 yenye namba za usajili 5H-PWF iliyotokea Novemba 6, 2022 asubuhi wakati ikijaribu kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba ikiwa na watu 43 wakiwemo abiria 39, marubani wawili na wahudumu wawili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news