Kusini bega kwa bega na Samia mpaka kieleweke,wasema mamia ya vijana leo

NA DIRAMAKINI

MAKUNDI mbalimbali ya vijana Mkoa wa Lindi yameungana kwa pamoja kufanya maandamano leo Novemba 30, 2022 katika hali inayoonesha kufurahishwa kwao na ujio na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya mkoa wao.
Vijana zaidi ya elfu moja (1000) waliovalia na sare zenye maudhui yenye kumshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa saa kadhaaa wameusimamisha mji wa Lindi kwa mbwembwe, vifijo na mabango yenye jumbe mbalimbali.

"Kusini bega kwa bega na Samia mpaka kieleweke"

Huu ni moja ya ujumbe maarufu uliotawala mabango yalioshikwa na vijana hao, wakijinasibu kutoa ushirikiano kwa Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news