MAMBO 10 YALIYOFANYIKA NDANI YA MUDA MFUPI WA UONGOZI WA RAIS SAMIA

NA ABDULAZACK ABDUL

MWAKA huu Benki ya Dunia imetoa ripoti iliyoangazia ukuaji wa uchumi, ongezeko la idadi ya watu, hali ya ustawi wa maisha ya watu, usawa wa kijinsia, mabadiliko ya tabia nchi na mambo mengine mengi.

Ripoti ile imenifanya nitafakari baadhi ya mambo yaliyofanywa kwa weledi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, twende pamoja;

1.Kuimarisha Uchumi:-Ukuaji wa pato la taifa katika robo ya pili mwaka 2021, uchumi uliongezeka kufikia asilimia 4.3, ukilinganisha na asilimia nne mwaka 2020.

Aidha, Sertikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia, imeweza kudhibiti mfumuko wa bei chini ya asilimia tano huku akiba ya fedha za kigeni ikiongezeka zaidi.

2.Kuchochea Biashara:-Maboresho ya sheria na miongozo mbalimbali yamefanyika na hivyo kuvutia wawekezaji kutoka katika kila pembe ya Dunia huku uuzaji wa bidhaa (export) ukiongezeka mara dufu.

Hivi karibuni tumeshuhudia makubaliano ya uwekezaji wenye thamani ya takribani shilingi trilioni 19 ikitarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 200,000.

3Kukuza Utalii na kuitangaza nchi yetu:-Katika hili Mheshimiwa Rais Samia ameweka rekodi ya aina yake hususani katika programu maalum ya TANZANIA:THE ROYAL TOUR ambayo imefanya miji kama Arusha kufurika kwa watalii.

4.Kuendeleza miradi ya kimkakati:-Mheshimiwa Rais Samia katika hili ameonesha umahiri na uwezo mkubwa ambapo mpaka sasa miradi yote inaendelea kama ilivyopangwa, huku miradi kama Reli ya Kisasa (SGR) ya Mwanza - Isaka ikitengewa zaidi ya shilingi trilioni moja kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

5.Kuimarisha Sekta ya Kilimo na Ufugaji:- Rais Samia ametatua changamoto nyingi za wakulima na kufungua masoko ndani na nje ya nchi.

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, zilipatiwa zaidi ya shilingi Bilioni 129 kununua mazao ya wakulima. Msamaha katika malighafi muhimu kwa wakulima kama vile mbolea na mpango wa ruzuku.

6.Kukuza Diplomasia:-Rais Samia ameirudisha nafasi ya Tanzania katika mawanda ya diplomasia za kikanda na kimataifa ikiwemo kushirikiana na mataifa mengine na pia kufungua Balozi mpya katika nchi wabia wa kibiashara na nchi yetu.

7.Kuboresha huduma za jamii:- Rais Samia amefanya makubwa kuhakikisha huduma za afya, maji, elimu, umeme na miundombinu zinaboreshwa kila uchao.

Hivi sasa tunatarajia hapo mwakani kila mwanafunzi aliye faulu darasa la saba aanze shule moja kwa moja.

8.Kuboresha sekta ya madini:-Katika sekta hii Mheshimiwa Rais amewezesha utoaji wa leseni zaidi ya 7900, huku viwanda vya uchakataji madini vikiendelea kujengwa na sekta hii ikichangia pato la Taifa kwa takribani asilimia 7.7.

Hivi karibuni Serikali inakwenda kuongeza umiliki katika Mgodi wa Almasi wa Mwadui Shinyanga. Juhudi hii ni kubwa.

9.Kuhakikisha Amani na Usalama:- Kama Amiri Jeshi Mkuu, Rais Samia ameweza kusimamia vema amani na usalama wa nchi yetu licha ya hali tete kwa baadhi ya nchi jirani, umakini na uongozi wake thabiti ndio sababu ya mafanikio haya.

10.Ajira na fursa kwa watumishi:- Rais Samia ametoa vibali vingi vya ajira serikalini, ametoa fedha za malimbikizo ya madeni kwa watumishi, vibali vya kupandisha madaraja kwa wenye sifa na zaidi ameondoa tozo (VRF) asilimia sita ya Bodi ya Mikopo na zaidi nyongeza ya mshahara.

Napenda kuchukua fursa hii kuungana na watanzania wote kumpongeza Rais wetu na kumtia moyo kwa kazi nzuri anayoifanya kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu. HISTORIA ITAMKUMBUKA kwa utofauti sana.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS WETU

Post a Comment

1 Comments