Mheshimiwa Sagini amshukuru Rais Samia kwa kuwapa heshima askari nchini

NA DIRAMAKINI

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Jumanne Sagini ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mageuzi makubwa kwa vikosi vyote vya ulinzi na usalama.
Ambapo hatua hiyo njema ni sehemu ya kuimarisha amani na usalama kwa wananchi na kuwafanya waendelee kufanya kazi mbalimbali za maendeleo na uzalishaji mali kwa ufanisi.
Mheshimiwa Sagini ameyasema hayo mkoani Mwanza katika Wilaya ya Ukerewe wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango.

"Napenda kutoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwajali askari wetu kwa kuwapandisha madaraja kwa kipindi cha miaka miwili,"amesema Mheshimiwa Sagini.
Aidha, Naibu Waziri Mheshimiwa Jumanne Sagini, ameishukuru Serikali kwa kutoa kiasi cha shilingi mil. 16. ili kuondoa makato kwa askari pindi wanapokuwa mafunzoni.

Mheshimiwa Sagini, amewasihi Watanzania wote kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news