Jeddah yakaribisha walioathiriwa na mafuriko waweze kulipwa fidia

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Jiji la Jeddah katika Ufalme wa Saudi Arabia umezitaka mamlaka za Serikali za mitaa kutumia utaratibu ule ule uliotengenezwa kufuatia mafuriko makubwa ya Novemba 2009 kulipa fidia kwa waathiriwa wa mvua kubwa iliyonyesha Alhamisi ya wiki hii.

Jeddah ni mji wa bandari wa Saudi Arabia kwenye Bahari Nyekundu na ni kitovu cha kisasa cha kibiashara na lango la mahujaji kwenye miji mitakatifu ya Kiislamu ya Makka na Madina.

Hayo yamesemwa na msemaji wa meya wa jiji hilo, Muhammad Al-Baqami wakati akitoa taarifa kuhusu walioathiriwa na mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha.

Amesema, watu walioathiriwa na mvua hiyo watawasilisha maombi yao katika Kituo cha Migogoro na Maafa, ambacho kinawakilisha mashirika yote ya Serikali ili kutathmini uharibifu na kuchukua hatua za kisheria ipasavyo.

"Mtu aliyeathiriwa na mvua ana haki ya kupata fidia kupitia sera za bima ikiwa ni pamoja na bima ya kubwa kwa uharibifu unaosababishwa na majanga ya asili, ikiwa ni pamoja na mvua, baada ya kesi kusajiliwa na mamlaka husika,"amesema.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Saudi Arabia, Al-Baqami amesema, fidia hiyo itapangwa na kamati zilizoidhinishwa na serikali, kwa mujibu wa Kifungu cha 27 cha Sheria ya Msingi ya Utawala, ambayo inasema kwamba serikali inahakikisha haki za raia na familia zao katika hali yoyote ya dharura.

Pia kamati zitaundwa, zikiongozwa na mkuu wa eneo, kupokea maombi ya waathiriwa wa mafuriko, kutathmini uharibifu na kuyawasilisha kwa Wizara ya Fedha baada ya kuidhinishwa na mamlaka inayohusika kwa ajili ya fidia. (Mashirika)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news