Mke anaruhusiwa kuuza mali ya mume wake bila kutaarifu ili kujipatia mahitaji

NA BASHIR YAKUB

KIFUNGU cha 64 cha Sheria ya Ndoa kinasema pale ambapo mume ameshindwa kutoa matunzo kwa mke wake basi mke huyo anayo mamlaka ya kuuza mali yoyote ya umme wake, lakini inayohamishika ili kujipatia mahitaji muhimu.Mali inayohamishika ni kama gari, pikipiki, samani, runinga na nyinginezo.

Mahitaji muhimu ni kama chakula, mavazi, afya, na malazi (sehemu ya kuishi/kodi). Aidha, si kuuza tu bali kifungu hiki kinasena anaweza kuitumia kukopea au kuitumia kwa namna nyingine yoyote ambayo itampatia mahitaji hayo muhimu.

Na anaruhusiwa kufanya hivyo si kwa mahitaji yake peke yake bali pia kwa mahitaji muhimu ya watoto.

Mke anaweza kufanya hivyo kama bado anaishi na huyo mume, na hata kama haishi naye tena, mathalani, wametengana, lakini kuna makubaliano ya kuendelea kumtunza mke, au wakati ambapo mume kaondoka nyumbani na kamtelekeza mke, au mke kaondoka kwa mume lakini kwa sababu ya matendo maovu ya mume huyo.

Hata hivyo, mke haruhusiwi kufanya hivyo ikiwa itathibitika kuwa anaishi na mwanaume mwingine. Kuna watu mtaona ukakasi kwenye jambo hili, lakini ndiyo hivyo mkasome kifungu hiki kipo na mtaona hii habari. Mwandishi wa makala hii ni Wakili anapatikana kupitia simu +255 714 047 241.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news