Yanga SC yategeshewa milioni 20/- za kuwamaliza

NA DIRAMAKINI

KAMPUNI ya Silent Ocean ambao ni wadhamini wa Tanzania Prisons ya jijini Mbeya wametoa ahadi ya shilingi milioni 20 kwa wachezaji wa timu hiyo ikiwa watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Yanga SC.

Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao unatarajiwa kupigwa Desemba 4, 2022 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Ahadi hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tu timu nyingine kutokea wilayani Mbarali mkoani Mbeya ya Ihefu FC kuwapoka Yanga alama zote tatu kwa mabao 2-1 baada ya kupigwa 'pira msuli' katika dimba la Highland Estate lililopo wilayani humo.

Aidha, taarifa kutoka kwa mdhamini huyo zimesema, hata Tanzania Prisons ikitoka sare na Yanga SC watapewa nusu ya fedha hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news