Pambani Kuzoya aibuka mchezaji bora

NA MWANDISHI WETU

KIUNGO mshambuliaji wa Simba Queens, Pambani Kuzoya amechaguliwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Determine Girls kutoka Libya katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pambani, Novemba 2, 2022 alionesha kiwango bora kwenye mchezo huo ambao Simba Queens waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kurejesha matumaini ya kutinga nusu fainali.

Mtanange huo wa Kundi A, ulipigwa katika dimba la Stade Moulay Hassan (Stade Prince Héritier Moulay El Hassan) lililopo jijini Rabat nchini Morocco.

Kipindi cha pili baada ya kocha Charles Lukula kufanya mabadiliko ya kumtoa Vivian Corazone ilimfanya Pambani kushuka chini kucheza pamoja na Joelle Bukuru ambapo aliifanya safu yao ya kiungo kuwa imara huku wakizuia na kushambulia kwa pamoja.

Baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi, Pambani aliwashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano mkubwa waliompa hadi kufanikisha jambo hilo.

“Nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa, pia benchi la ufundi kwa kunipa nafasi ya kucheza ninaamini tutaendelea kufanya vizuri,”amesema Pambani.

Post a Comment

0 Comments