Simba Queens yawachapa Determine Girls mabao 2-0

NA MWANDISHI WETU

SIMBA Queens imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls kutoka Liberia katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mtanange huo wa Kundi A, ulipigwa Novemba 2, 2022 katika dimba la Stade Moulay Hassan (Stade Prince Héritier Moulay El Hassan) lililopo jijini Rabat nchini Morocco.

Mchezo ulianza kwa kasi huku,wakishambuliana kwa zamu lakini safu zote za ushambuliaji zilishindwa kutumia nafasi ilizotengeneza.

Kipindi cha pili Kocha Charles Lukula aliwatoa Asha Mnuka na Vivian Corazone na kuwaingia Amina Ahmed na Olaiya Barakat ambao waliongeza kasi kwenye safu ya ushambuliaji.

Opa Clement alitupatia bao la kwanza dakika ya 53 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Olaiya muda mfupi baada ya kuingia.

Kocha Lukula aliwaingiza pia Dotto Evarist na Philomena Abakah kuchukua nafasi za Silvia Mwacha na Asha Djafar ambao nao waliifanya timu kuwa imara zaidi.

Olaiya aliwapatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 79 baada ya Joelle Bukuru kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Nahodha wa Determine Margaret Stewart alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Opa dakika ya 88.

Mchezo wa Simba Queens wa mwisho wa hatua ya makundi utakuwa Jumamosi Novemba 5 dhidi ya Green Buffaloes kutoka Zambia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news