Rais Samia aipa kongole Yanga SC kwa kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam kwa kutinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

"Kongole Yanga SC kwa ushindi na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya soka la wanaume kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, msimu wa 2022/2023. Nawatakia kila la kheri katika hatua inayofuata;

Mheshimiwa Rais Samia ametoa pongezi hizo leo Novemba 10, 2022 kupitia mitandao yake ya kijamii ikiwa ni siku moja baada ya Yanga SC kupata mafanikio hayo.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara walitinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Novemba 9, 2022 baada ya kuichapa bao 1-0 wenyeji Club Africain kupitia mchezo uliopigwa katika dimba la Le stade olympique de Rad├Ęs jijini Tunis nchini Tunisia.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Yanga, Stephane Aziz Ki ndiye shujaa wa klabu hiyo ambapo akitokea benchi aliipatia bao muhimu timu yake dakika ya 79 akimalizia pasi ya Fiston Mayele.

Awali dakika 45 zilitamatika kwa timu zote mbili ubao kusoma sufuri, baada ya miamba hiyo kuoneshana soka la hali ya juu.

Post a Comment

0 Comments