Rais Samia ashiriki Mkutano wa Kujadili Mabadiliko ya Tabianchi COP27 nchini Misri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Wakuu wa nchi mbalimbali kabla ya kuanza kwa Mkutano wa kujadili mabadiliko ya Tabianchi COP27 unaofanyika katika Mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri leo Novemba 7, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Malawi, Mhe. Lazarus Chakwera katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh International Congress Centre.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres (kulia) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa COP27 unaofanyika katika Mji huo nchini Misri leo Novemba 7, 2022.

Post a Comment

0 Comments