Rais Samia atunukiwa tuzo ya Uongozi wa Kimageuzi barani Afrika 2022

NA MWANDISHI WETU

HATIMAYE RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa Tuzo ya Uongozi wa Kimageuzi barani Afrika (African Leadership Award 2022) kutoka Taasisi ya Afrimma ya mjini Dallas, Marekani kwa kutambua mchango wake katika sanaa nchini Tanzania.
Tuzo hiyo imepokewa kwa niaba ya Rais Samia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi, usiku wa kuamkia leo mjini Dallas ambapo mwakilishi huyo amesema Rais Samia katika kipindi kifupi cha uongozi wake amefanya mageuzi mengi katika sekta ya sanaa ikiwemo kurejesha tuzo za muziki na kuboresha mifumo ya mirabaha ili kuwainua wasanii.

Awali mamia ya mashabiki waliohudhuria tuzo hizo walimshangilia kwa nguvu Rais Samia alipoonekana katika baadhi ya vipande vya filamu ya Royal Tour vilivyokuwa vikioneshwa kabla ya kutolewa tuzo hiyo.

Viongozi wengine wakuu wa Afrika waliowahi kutwaa Tuzo hiyo ni Rais Ian Khama wa Botswana (2015) na Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria (2017).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news