TENDEA HAKI WENGINE

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa, unapomalizika Mwaka C wa Liturjia ya Kanisa kuelekea Mwaka A ikiwa pia dominika ya Kristo Mfalme ni muda sahihi wa kujipima kila mmoja kama amelitendea haki kanisa na kuwatendea haki wengine.

Hayo yamehubiriwa katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Jumapili ya leo Novemba 20, 2022, Parokia ya Chamwino-IKulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma na Padri Paul Mapalala.

“Katika kipindi chochote cha miaka tulicho nacho, wengine mwaka mmoja, wengine miaka 100 na kadhalika, tukipima katika kipindi kizima cha Mwaka C, Je umelitendea haki kanisa? Je umeitendea haki familia yangu? Je umeitendea haki jumuiya yako? Je umewajibika kiserikali kama mtumishi ? Je umewajibika hata kwa chama chochote ulichonacho cha kitume na vyama vingine ? ”.

Akiendelea kuhubiri Padri Mapalala amesema kuwa,“Kipimo chochote kinachofikiwa, tunapaswa kumkabidhi Kristo kama alivyofanya huyo aliyesubiwa na Yesu Kristo msalabani, hapo tuseme, ‘Bwana wetu Yesu Kristo samahani kwa yote ninaomba nianze kipindi kipya cha mwaka upya.’ .”

Misa hiyo pia iliambatana na maombi matano na mojawapo lilikuwa hili, “Utukumbushe kwamba maisha ya duniani yanakwisha na kwamba tumeumbwa kuishi milele katika heri ya uzima wa milele, Ee Bwana.”

Katika misa hiyo mara baada ya waaamini walikuwa wamejiandaa kukomunika Padri Mapalala na frateli walirudi Altareni wakijiandaa kupeleka Ekaristi Tabenakuo, gafla mama mmoja mzee alinyanyuka na kwenda Altareni ili aweze kupokea, jambo kidogo lilishangaza waamini, je hakuona wakati waamini wakipokea? Mama mzee aliongozwa na mlei mmoja na frateli akamfuata na kumkomunisha mama huyu na baadaye mama yetu huyu kurudi alipokuwa ameketi.

Mwandishi wa ripoti hii alibani kuwa mama huyu uzee wake ikiwamo uoni hafifu ndiyo uliomsabisha achelewe kuona kama waamini walishapokea na mwandishi aliona pia umuhimu mkubwa wa wazee kuishi nao kwa karibu sana kama watoto popote walipo.

Hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu imebadilika huku sasa manyunyu ya mvua yakianza na anga limebadilka kuwa na mawingu kiasi. Wakulima wakijiandaa kuzisaka mbegu zilipo kuziweka tayari zikapandwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news