RAIS WA YANGA SC ATOA TAMKO NZITO

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Yanga SC, Mhandisi Hersi Said amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kutozingatia kejeli zinazoendelea mitandaoni zikihusisha kauli yake aliyoitoa jijini Mwanza wakati timu hiyo ikijiandaa kumenyana na Geita Gold kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mhandisi Hersi Said ameyasema hayo Novemba 3,2022 kupitia chaneli yao ya Yanga Tv jijini Dar es Salaam.

”Wote waliosikiliza kauli yangu wanaelewa nilikuwa namaanisha nini. Ni kauli ambayo ilikuwa inajenga mapenzi na klabu na sio mapenzi na matokeo ya klabu,” amesema.

Rais huyo pia amesema wamepokea maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa na wapenzi wa timu hiyo kutokana na matokeo waliyoyapata jana kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain.

“Wapo baadhi ya watu wasioitakia mema klabu yetu wametumia kauli yangu ambayo nilitumia wakati nazungumza na viongozi wa matawi mkoani Mwanza wakiitumia kauli ile kuwakejeli mashabiki wa timu yetu.

“Nataka niwahakikishie uongozi wenu ni uongozi ambao ni sikivu sana, lakini umekuwa karibu na wanachama wa kila aina nikiwemo mimi kama Kiongozi wa klabu hii nimekuwa nikifika katika kila aina ya maeneo ikiwemo maeneo ya watu wenye uhitaji sana. Na nimekuwa nikisikiliza na kuheshimu watu wa aina zote.

“Naomba wanachama na wapenzi wa Young Africans wapuuze kejeli zinazotumia sura yangu katika kuonesha kejeli hizo kwa wanachama,"amesisitiza Mhandisi Said.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news