RHMT Dodoma yashauriwa kutumia chumba cha uchakati takwimu kufanya maamuzi

NA ASILA TWAHA,OR-TAMISEMI

TIMU ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ngazi ya Mkoa ( RHMT) imeshauriwa kuwa na tabia ya kutumia chumba cha kuchakata takwimu ( Situation Room) ili kufanya maamuzi sahihi yatakayopelekea uboreshaji na uimarishaji wa huduma za afya nchini.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 10, 2022 jijini Dodoma katika mafunzo ya kutumia takwimu katika chumba cha uchakataji ( Situation room) kwa RHMT Mkoa wa Dodoma.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Ufundi Mradi wa Data For Implementation Bw.Jackson Ilangali ambae amesema kuwa ili kuleta matokeo chanya katika sekta ya afya lazima kutumia taarifa na takwimu sahihi ambazo zinaendana na uhalisia wa huduma inayotolewa pamoja na wananchi wanaopata huduma hiyo.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo RHMT jinsi ya kutumia chumba cha uchakataji takwimu ( SITUATION ROOM) katika kufanya maamuzi sahihi ili kuendelea kuboresha utolewaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Kwa upande wake Mtakwimu Ofisi ya Rais TAMISEMI (Idara ya Afya), Bi. Anna Ndakidemi ametoa rai kwa wataalamu hao kutumia chumba cha uchakataji wa takwimu sababu amesema chumba hicho kikitumiwa vizuri Serikali itapanga mahitaji ya huduma za afya kwa wananchi kutokana na takwimu sahihi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news