NA DIRAMAKINI
MABINGWA watetezi, Young Africans SC,(Yanga SC) wanaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/2026 baada ya kufikisha pointi 28 katika michezo 10 waliyocheza. Timu hiyo imeonesha ubora mkubwa kwa kushinda mechi tisa na kutoka sare moja, ikifunga mabao 27 na kuruhusu mawili pekee.
JKT Tanzania wanashika nafasi ya pili pia wakiwa na pointi 28, lakini wamecheza michezo 17. Simba SC wanashika nafasi ya tatu kwa pointi 23 baada ya kucheza michezo 10, wakifuatiwa na Pamba Jiji wenye pointi 23 katika michezo 14. Azam FC wanashika nafasi ya tano kwa pointi 22.
Katika eneo la hatari, KMC FC wapo mkiani wakiwa na pointi nane baada ya michezo 16, huku Fountain Gate na Tanzania Prisons wakihitaji kujipanga zaidi kujinasua kwenye mstari hatari.
