Simba SC, Singida Big Stars walazimishana sare bao 1-1

NA DIRAMAKINI

SINGIDA Big Stars wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Wenyeji hao ambao wameikaribisha Simba SC ya jijini Dar es Salaam katika Dimba la Liti (Namfua Football Ground-Namfua Stadium) lililopo mkoani Singida wameonesha soka safi.

Mtanange huo umepigwa leo Novemba 9, 2022 ambapo kiungo mshambuliaji, Deus Kaseke alianza kuifungia bao Singida Big Stars dakika ya 11.

Aidha, Simba SC baada ya bao hilo waliongeza presha langoni mwa Singida, lakini walikosa utulivu wa kumalizia nafasi walizotengeneza.

Bao hilo ambalo lilidumu kipindi chote cha kwanza, licha ya wenyeji hao kuendelea kulilinda kipindi cha pili winga Peter Banda aliisawazishia bao hilo dakika ya 58 muda mfupi baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Jonas Mkude akimalizia pasi ya Moses Phiri.

Post a Comment

0 Comments