Simba Queens yaondoka na milioni 440/- Ligi ya Mabingwa Afrika

NA DIRAMAKINI

SIMBA Queens ya jijini Dar es Salaam, Tanzania imeaga katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuandika historia ya kufuzu nusu fainali.

Tamati yao imefikia leo Novemba 9, 2022 baada ya kuchapwa bao 1-0 na mabingwa watetezi, Mamelodi Sundown katika dimba Prince Moulay EL Hassan jijini Rabat nchini Morocco.

Bao pekee la Mamelodi Sundown limefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Lesotho, Boitumelo Joyce Rabale dakika ya 76 akimalizia kazi nzuri ya nyota wa Banyana Banyana, Melinda Kgadiete.

Nusu Fainali ya pili inafuatia baina ya wenyeji, FAR Rabat na Bayelsa Queens ya Nigeria katika dimba hilo la Prince Moulay EL Hassan.

Katika mtanange huo, Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula alifanya mabadiliko matatu ya kikosi kwa kuwaanzisha Vivian Corazone, S’arrive Lobo na Koku Ally ambao hawakuanza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Green Buffaloes.

Nyota Pambani Kuzoya, Olaiya Barakat na Amina Hemed ambao mchezo uliopita walianza leo wameanzia benchi ambapo kikosi kamili kilikuwa namna hii, Gelwa Yona (21), Fatuma Issa (5), Diana Mnali (15), Daniela Kanyanya (22), Violet Nicholas (26), Joelle Bukuru (18), Vivian Corazone (4), S’arrive Lobo (2), Koku Ally (19), Opa Clement (7)Asha Djafari (24).

Wachezaji wa akiba walikuwa ni Zubeda Mohamed (20), Janeth Simba (1), Dotto Evarist (11), Wema Maile (3), Jackline Albert (16), Topister Situma (13), Pambani Kuzoya (17), Amina Hemedi (14), Olaiya Barakat (9).

Aidha, kwa kuishia nusu fainali, Simba Queens itazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani 200,000 (zaidi ya shilingi milioni 440 za Kitanzania) akati bingwa atapata dola 400,000 na mshindi wa pili dola 250,000.

Wakati huo huo, timu mbili zilizomaliza nafasi ya tatu katika makundi kila mmoja atajinyakulia dola 150,000 kila moja na nyingine mbili zilizoshika mkia dola 100,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news