Waziri Mchengerwa atoa wito kwa wakuu wa mikoa kuhusu michezo na sanaa

NA JOHN MAPEPELE

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wakuu wa mikoa wote nchini kuhamasisha shughuli za michezo na sanaa ili kuibua vipaji na kuimarisha afya zao.
Waziri Mchengerwa ametoa wito huo usiku wa Novemba 12, 2022 kwenye hotuba yake ya kufunga mashindano ya Kikapu ya Kombe la CRDB jijini Tanga.

Amesema, kwa upande wa Serikali, tayari imepanga kukarabati viwanja saba ikiwa ni maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya AFCON 2027.
"Tunatamani kuona kila wilaya kuwe na kiwanja na kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatekeleza Sera ya Utamaduni,"amefafanua Mhe.Mchengerwa.


Aidha, ametoa wito kwa halmashauri zote nchini kutenga maeneo na fedha kwa ajili ya kujenga viwanja vya kisiasa vya michezo.
Amewataka kuandaa mpango wa kazi ili kuona ni namna gani wizara inavyoweza kusaidia utekelezaji wake.

Awali Waziri Mchengerwa alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na hamasa kubwa anazozitoa kwenye sekta za michezo hali ambayo imesaidia kuleta mafanikio makubwa katika kipindi kifupi cha utawala wake.
Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na timu za soka za Serengeti Girls na Tembo Warriors kufuzu robo fainali Kombe la Dunia,kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani ambapo Tanzania ilishinda.

Mengine ni wachezaji 10 wa Tembo kusajiliwa vilabu vya kimataifa barani Ulaya wakati wachezaji sita wa Serengeti Girls wamepata nafasi ya majaribio nchini Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news