Waziri Mchengerwa: Tamasha la Bagamoyo limemalizika kwa mafanikio makubwa

NA JOHN MAPEPELE

TAMASHA la Kimataifa la 41 la Utamaduni na Sanaa -Bagamoyo 2022 lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philipo Mpango limemalizika kwa mafanikio makubwa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa siku ya mwisho wa tamasha ambapo amefafanua kuwa kumekuwa na maboresho makubwa ikilinganishwa na matamasha yaliyopita.

Aidha, amesema Wizara yake kwa kushirikiana na wadau itaendelea kuboresha Tamasha hili ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

0 Comments