Waziri Prof.Mkenda agusia somo la Kiarabu katika tahasusi

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amepokea pendekezo lililotolewa na wamiliki wa shule za Kiislamu kuhusu namna ya kuangalia uwezekano wa kuingiza somo la Kiarabu katika tahasusi za masomo ya elimu ya juu hapa nchini.
Prof.Mkenda ameyasema hayo leo Novemba 6, 2022 wakati wa Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika katika uwanja wa Garden uliopo Masjid Taqwah Ilala Bungoni, Dar es Salaam. Mahafali hayo yamejumuisha shule zaidi ya 10 kutoka Kanda ya Mashariki.

"Yale mengine mliyoyasema ni combination (tahasusi) kuwe na combination (tahasusi) mojawapo ya Kiarabu kwenye shule za Serikali.

"Kiarabu kinafundishwa na dini ya Kiislamu na ni lugha ya kwanza kutoka nje ya eneo letu kuingia hapa ya kigeni. Hatuwezi tufundisha Kifaransa, Kiingereza, Kichina halafu Kiarabu tukaacha kufundisha si kwamba tu tutakuwa tunawekeza kwenye jambo ambalo litasaidia kwenye imani yao.

"Kwa kweli itatusaidia sisi kuandaa watu ambao watatumia Kiswahili kama wakalimani, utakuwaje mkalimani kama hujui lugha nyingine, lazima ujue lugha kadhaa, na lugha ya Kiarabu ni lugha nadhani ya pili au ya kwanza inayozungumzwa katika bara la Afrika, ni lugha namba mbili ya dunia katika Umoja wa Mataifa.

"Kwa hili nakwenda nalo, nakwenda kutafuta shule ambayo tunaweza kuanza nayo mara moja ili tuwe na combination katika shule za Serikali ambayo kuna kuwa na somo la Kiarabu kama somo la kufundisha,"amefafanua Prof.Mkenda.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkenda akijibu ombi la Serikali kuangalia uwezekano wa somo la dini kupewa msukumo sawa na masomo mengine shuleni, amewaomba viongozi hao kuvuta subira kwanza.

"Hili la kufundisha dini tuliache katika mjadala...kwamba mtu anapochukua somo la dini liwe katika masomo yanayohesabika, kuna sababu kadhaa lazima tulizingatie kwa sasa siwezi kulizungumzia.

"Jambo jingine ni kuhusu vibali vya kufungua shule, kweli changamoto mijini ni ardhi, hili tutaanza kuliangalia upya kwamba si lazima eneo liwe kubwa sana pengine lazima uende juu. Najua kuna changamoto shule moja katika mkoa fulani ilikuwa inatakwa kufungwa...lakini baada ya kujionea nilitoa maelekezo, maana walikuwa wameshaanza, sasa haikuwa busara kusitisha masomo.

"Hivyo, yeyote anayetaka kuanzisha shule hapa mjini kwa masharti yetu inaweza kuwa changamoto lazima masharti yatabadilika kuwa vertical au horizontal expansion kwa ujumla wake,kwa hiyo tuendelee kushirikiana ninaamini kwa Serikali hakuna linaloshindikana,"amesema Waziri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news