Waziri Mkuu awasili mkoani Kagera kushuhudia zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia Ndege ya Precision Air kupata ajali, awataka wananchi kuvuta subira

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumapili Novemba 6, 2022 amewasili mkoani Kagera kushuhudia zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia Ndege ya Precision Air kupata ajali ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewajulia hali wahanga wa ajali hiyo wanaopata matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera.
Akizungumza katika eneo hilo, Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatoa pole kwa wote walioguswa na ajali hilo na kwamba Serikali itaendelea kutoa huduma stahiki kwa majeruhi wote.

Pia, amewataka wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ambacho Serikali itafanya uchunguzi kupitia vyombo vyake ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Post a Comment

0 Comments