Waziri Simbachawene ahimiza mafunzo ya Itifaki kuwa endelevu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amesema ipo haja mafunzo ya itifaki na uratibu wa maadhimisho kufanyika kila mwaka.
Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya itifaki na uratibu wa maadhimisho/sherehe na matukio ya kitaifa.(Picha na OWM).

Wito huo umetolewa Novemba 19, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene wakati akifunga mafunzo kwa watendaji wa Serikali yaliyohusu itifaki ya viongozi wa kitaifa iliyowakutanisha Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa yaliyofanyika mkoani Singida.
Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania,Profesa Elisante Ole Gabriel kabla ya kufunga mafunzo.

“Mafunzo haya yanapaswa kuongezwa mada na kuongeza namba ya washiriki ili kujenga uelewa wa pamoja,”amesema.

Waziri Simbachawene amesema, utaratibu huo utasaidia kupata ufahamu na ujuzi muhimu wa namna ya uandaaji wa maadhimisho yanayohusu Idara na Taasisi za Serikali kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa na kuzijua kanuni za kiitifaki ambazo mtazitumia katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali kwenye taasisi zenu.
Washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo ya itifaki na uratibu wa maadhimisho zikiwemo sherehe na matukio ya kitaifa yaliyowahusisha Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa.

Awali Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw. Kaspar Mmuya amesema mafunzo yamelenga kuwa na utaratibu ambao umekubaliwa, ambao unaleta matokeo chanya na watu wote kuheshimu.

“Watendaji waliopokea mafunzo sasa watasaidia katika maeneo yao; kitengo cha maadhimisho Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa sababu ndio ofisi inayosimamia itifaki za viongozi”.
Washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo ya itifaki na uratibu wa maadhimisho ikiwemo sherehe na matukio ya kitaifa yaliyowahusisha Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel aliyekuwa mtoa maada wa huduma bora kwa mteja ameshukuru serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yamesaidia kuwajenga watendaji kwenda kwa muelekeo unaolengwa na nchi.

“Huu ni uwekezaji wa kifikira unaofaa, watendaji wakitoa huduma bora kwa wananchi na kwa viongozi, mashauri yatapungua kwa sababu ya huduma kuwa nzuri,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news