Wizara ya Elimu yawaongezea maarifa viongozi, watumishi

NA MWANDISHI WETU

KATIKA kuimarisha utendaji Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatoa mafunzo kwa viongozi na watumishi juu ya masuala ya itifaki kwa lengo la kuwajengea uwezo.
Akifungua mafunzo hayo jijini Dodoma Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Francis Michael amewataka viongozi na watumishi hao kuhakiksha wanashiriki kikamilifu ili matokeo ya mafunzo hayo yaweze kuonekana katika utendaji.

"Nimezisikia mada ambazo mtakwenda kufundishwa zote ni muhimu na zina tija katika kuimarisha utendaji na utoaji huduma kwa wateja ndani na nje ya wizara, hakikisheni mnashiriki kikamilifu,"amesema Dkt. Michael.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Moshi Kabengwe amesema mafunzo hayo yamejumuisha washiriki 147 ambao ni Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Makatibu Mahsusi, Watunza Kumbukumbu na baadhi ya Wathibiti Ubora wa Kanda na Wilaya.
Ametaja mada zitakazowasilishwa katika kikao hicho kuwa ni masuala ya Itifaki, Mawasiliano fanisi ndani na nje ya Wizara, Misingi ya utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka pamoja na Utendaji wa pamoja (team work).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news