Argentina yatinga nusu fainali kwa kuichapa Uholanzi

NA DIRAMAKINI

UBORA wa mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Argentina (La Albiceleste),Emiliano Martinez umeliwezesha Taifa lake kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) 2022 nchini Qatar.

Mlinda mlango Emiliano Martinez wa Argentina akiokoa mkwaju wa penalti uliokosa na Virgil van Dijk wa Uholanzi wakati wa muda wa mikwaju ya penalti. (Picha na Paul Childs/Reuters).

Ni baada ya Martinez kuokoa mara mbili mikwaju ya moto kupitia mtanange wa nguvu dhidi ya Uholanzi uliopigwa Desemba 9, 2022 katika Uwanja wa Lusail nchini Qatar na kutinga nusu fainali.

Aidha, Lautaro Martinez alifunga penalti ya ushindi wakati Argentina ilipomaliza pambano la dakika za lala salama kutoka kwa Uholanzi.

Argentina walikuwa wametangulia kwa mabao 2-0 kwa maana ya lile la Nahuel Molina dakika ya 35 na la Lionel Messi dakika ya 73 kwa penalti zikiwa zimesalia dakika 17 mechi kumalizika.

Lakini Wout Weghorst aliyetokea benchi alifunga dakika ya 83 na kusababisha mchezo kwenda katika muda wa ziada ambapo dakika ya 101 alipachika bao la pili.

Huku kukiwa hakuna bao la ziada katika dakika 30 za muda wa nyongeza, mechi iliamuliwa kwa mikwaju ya penalti, huku Wamarekani hao wa Kusini wakishinda 4-3.La Albiceleste sasa itamenyana na Croatia kwenye Uwanja wa Lusail siku ya Jumanne ijayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news