MIAKA 61 YA UHURU:Waziri Simbachawene asema nchi imepiga hatua

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amesema nchi imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa maendeleo ambayo ni shirikishi na yamelenga watu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara kilichofanyika Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

“Katika ujenzi wa maendeleo ukisema ujenzi wa sekondari za kata, ujenzi wa vituo vya afya ujenzi wa barabara vyote vimetekelezwa kwa kushirikisha wananchi.”

Kauli mbiu ya miaka 61 ya Uhuru ambayo inasema, "Amani na Umoja ni nguvu ya maendeleo yetu.” Imetusaidia kutimiza shabaha zetu.

“Mabadiliko ya kisiasa, mabadiliko ya kiuchumi, Mhe. Rais amepeleka maendeleo hayo kwa watu na maendeleo ya watu yanahitaji rasilimali fedha,”amesema Waziri Simbachawene.

"Sisi watanzania tuna misingi yetu kila awamu inayoingia inategemea misingi ya awamu iliyopita ndio maana tumefika hapa tulipofika.
“Watanzania wanapenda furaha watanzania hawapendi hofu watanzania ni watii kwa mamlaka, tuendelee kuheshimiana na kuipenda nchi yetu.”

Hata wenye mawazo mbadala Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefungua mipaka ndio maana anazungumzia R-nne watu wawe na utaratibu wa maridhiano; maelewano, kujenga upya, na kuendelea mbele.

“Tunaiona Tanzania iliyobadilika sana kimaendeleo, lakini imebakia na misingi ile ile iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu katika mioyo ya watu.”

"Tulivyopata uhuru falsafa ya Baba wa Taifa alisema, Uhuru ni kazi ndio maana wananchi wamejikita katika kufanya kazi."

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. George Fuime amesema, nchi imepiga hatua kwenye miundombinu ya mawasiliano.

“Ujenzi wa miundombinu ya afya, ujenzi wa miundombinu ya elimu, mabadiliko haya yameasisiwa na viongozi wetu kutokana na amani na utulivu uliojengwa na wazee wetu.”

Naye muwasilishaji mada Mwalimu Charles Malugu amesema, Serikali ya Awamu ya Sita imefanya ujenzi wa sekondari vyumba 20000, na ujenzi wa vyumba 3000 kwa shule shikizi ambao utasaidia wanafunzi wa kidato cha kwanza na wanafunzi wa darasa la kwanza kuanza masomo bila kuwa na kikwazo cha aina yoyote.

“Serikali ya awamu ya sita imeruhusu wanafunzi walikatisha masomo kutokana na ujauzito, kuendelea na masomo ili wasikatize ndoto zao.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news