BUNDI WA GAMBOSHI SEHEMU YA 59

NA WILLIAM BOMBOM

MGANGA aliendelea kuonja joto la jiwe, hakuamini kilichokuwa kikitokea mbele yake. Wakati huo BUNDI WA GAMBOSHI alikuwa akimalizia kula lile jicho la mganga alilolinyofoa.

Hapa niseme kidogo, wakati tunamchukua mganga kule kituo cha afya kitandani tuliacha mgomba uliokuwa na picha ya mganga.

Mgomba huo ulikuwa umepewa uhai wa muda mfupi ili kuondoa taharuki katika hospitali na ndugu wa mganga. Kuna muda huwa tunaweka mbwa, nyani, msukule au gogo, hutegemea na lengo la wachawi wenyewe.

Inapotokea katika familia yenu mkauguza mgonjwa kwa muda mrefu hospitali, mkatumia kiasi kikubwa cha gharama za kumtibu kisha akafa basi tambua mliyekuwa mkimuuguza hakuwa binadamu bali alikuwa nyani.

Mara nyingi hili huwa tunalifanya kuwakomoa familia husika, yaani wapoteze mali na mtu wao. Kwa mtu wa kawaida ni vigumu kulitambua hili, pia huwa tunaongezea madawa ya kuwafanya familia kuamini mgonjwa wao atapona kumbe sivyo.

Vipimo vingine huwa tunadanganya, kwa mfano mgonjwa anaweza kupimwa akaonekana ana Virusi Vya Ukimwi (HIV) kumbe sivyo.

Wakati wa kumpima wanapochukua sampuli ya vipimo huwa tunabadili na kuweka sampuli ya ugonjwa tunaoutaka na kuondoa sampuli yake.

Hapa ndipo huleta majibu yasiyo sahihi, ndiyo maana wagonjwa wa namna hii wengine hukimbilia misikitini na makanisani kuombewa.

Ndugu msomaji nadhani ulishawahi kusikia kuwa, mgonjwa kafanyiwa upasuaji halafu matabibu wakasahau mkasi au wembe ndani ya tumbo.

Kwa mafunzo ya matabibu kitu hiki ni vigumu sana kutokea, yaani jopo la matabibu wasahau mkasi? Kwa kifupi hili jambo huwa tunalifanya sisi wenyewe, wakati wa upasuaji huwa tumo ndani ya chumba husika.

Huwa tunautumia muda huo kufanya jambo lolote tupendalo, tunaweza kutumia mwanya huo kurudisha mkasi, wembe ama kisu ndani ya tumbo la aliyefanyiwa upasuaji. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunamtesa mgonjwa huyo kama atakuwa halisi na tumekubaliana kumuua.

Kwa upande wa mganga tulikuwa tumeacha kipande kidogo cha mgomba kitandani, kisha tukamchukua yeye na kumleta kambini hapo.

Hakukuwa na haja ya kuendelea kuwatesa familia yake kwa kuwawekea nyani, tulikuwa tumedhamiria kumuua kabisa tena kwa mateso.

Ghafla BUNDI WA GAMBOSHI alimrukia tena mganga, akazishika nyeti zake na kuzivuta kwa nguvu. Mganga aligugumia kwa maumivu makali, lakini BUNDI WA GAMBOSHI hakusita, zilivutwa nyeti zikachomoka zote zikiwa zimeshikana na kende.

Nilimsogelea yule mganga wakati huo akitapatapa, nikamkanyaga kwa nguvu sehemu ya jeraha la upasuaji. Mguu wangu ulizikata nyuzi ukazama ndani ya kifua cha mnganga huyo, punde si punde alikata roho mbele yetu.

BUNDI WA GAMBOSHI alinyanyua mbawa zake kisha akapigapiga hewani huku akimalizia kula nyeti za mganga.
Huu ulikuwa ushindi mkubwa kwa kambi yetu, kuuawa kwa mganga huyo ilifungua mango mpya wa kusikika kwa kambi yetu.

Niliutumia muda huo kuwaita wachawi waliokuwa chini yangu nakuwaagiza kubanika mwili wa mganga huyo. Wakati huo tulikuwa tumeshanyofoa maini, bandama na moyo.

Tulitia chumvi ikiwa mibichi kisha tukaanza kuila, ilikuwa mitamu kuliko maelezo. Mwili mwingine wa mganga huyo ilikwenda kubanikwa.

Tayari BUNDI WA GAMBOSHI alikuwa ameshamaliza kula zile nyeti za mganga, alizitoboa kende na kufyonza rojorojo yote iliyokuwa ndani ya kende.

Siku zilikwenda huku tukipambana na ujenzi wa GAMBOSHI MPYA, hakukuwa na kiumbe mwingine aliyekuwa akitusumbua tena.

Hatimaye tulikamilisha ujenzi huo, ilikuwa kambi kubwa ya kupendeza. Kambi ya kisasa iliyokuwa na majengo ya. kileo, hakuna kambi nyingine ya kichawi kwa ukanda wa ziwa magharibi iliyokuwa na hadhi ya namna hiyo.

Kwa kuwa kambi ilikuwa kubwa, kwa namna yeyote ile walitakiwa msukule wa kutosha. Kambi yeyote ya wachawi ni lazima iwe na misukule, hivyo misukule ndiyo kitambulisho cha ukubwa wa kambi yeyote.

Tulianza kuandaa mazingira ya kujaza kambi hiyo ya misukule, kwa kuwa ilikuwa ni kazi iliyohitaji vifo vya binadamu wengi ni vyema tungekaa kitako na kupangilia.Ndugu msomaji mambo yanazidi kwenda mbele, unadhani nini kinafuata? Endelea kufuatilia kisa hiki.

Pia ndugu msomaji usipitwe na simulizi ya KANISA LA KICHAWI na KABURI LA RAIS WA HOVYO zitakazoanza tarehe 1/1/2023

ULAKOMEYE?
THE BOMBOM

Post a Comment

0 Comments