CHADEMA,ACT Wazalendo wampokea Rais Dkt.Samia kwa shangwe Lindi

NA DIRAMAKINI

WAFUASI wa vyama vikuu vya upinzani nchini kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na ACT WAZALENDO Mnazi mmoja mkoani Lindi wameungana na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Wananchi katika mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea na ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kwa nyakati tofauti, wafuasi hao wameieleza DIRAMAKINI kuwa, dhamira ya kushirikiana na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watanzania wengine kwa umjumla inatokana na wao kuvutiwa na uongozi shirikishi, sikivu na jumuishi kupitia Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia.
Pia wameongeza kuwa, Rais Dkt,Samia katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameweza kuimarisha demokrasia, utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea na iliyokamilika vijijini na mijini ambayo imekuwa na matokeo chanya kwa ustawi bora wa uchumi wa jamii na Taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments