HAPANA NDIYO MAANA YAKE NDIYO

NA ADELADIUS MAKWEGA

TULIPOKUWA wadogo nyumbani kwetu Mbagala kulikuwa na mzee mmoja wa Kichaga aliyefahamika kama Benson Njiu maarufu kama Mzee Ben, kwa wale wageni wa Mbagala na wenyeji, nyumba ya mzee huyu ipo pale kilipo Kituo cha Mabasi cha Mbagala Mpili (Mbagala Sabasaba) kama unakwenda Mbagala ukishuka uwe kama unarudi ulipotoka, nyumba ya tatu hapo ndipo ilipo nyumba ya mzee wangu huyu.

Benson Njiu alizaliwa huko Moshi mkoani Kilimanjaro na kuhamia Mbagala, hapa alifunga ndoa na shangazi yake mwanakwetu bibi mmoja wa Kimatumbi-Binti Mkundi, tangu enzi hizo nyumba yake ilikuwa na duka lenye bidhaa kadhaa na kama unakwenda kununua kitu hapo ulitakiwa kwenda kwa nidhamu kinyume chake bidhaa usingeipata.

Mwanakwetu alizifaidi mno tabia za ndugu huyu kwa kuwa alikuwa akisali naye pamoja katika Kanisa la Mtakatifu Antony wa Padua hapo Mbagala Misheni, hilo ni kanisa moja dogo, zuri na kongwe. Kwa umri wa kanisa hilo sasa ni karibu mara mbili ya umri wa mwanakwetu.

Uzuri wa kanisa hili ni wa mambo mengi lina mabechi mazuri na imara ya mti wa Mninga na Mvule ya enzi hizo na mabechi hayo tangu yaingizwe humo hayajawahi kutolewa zaidi ya kupigwa msasa na polishi huku madirisha ya kanisa hilo ni yale ya kupanga vipande vya mbao na huwa vinaangukaanguka nao ukarabati ukifanyiwa kila mara.

Ndani ya kanisa hilo kuna kengele moja kubwa ambayo ikipigwa Mbagala nzima inasikika huku iliwahi kuwarusha juu akina mwanakwetu enzi hizo kutokana na uzito wake.

Altare ya kanisa hilo mkono wa kulia na kushoto kuna picha ya Mtakatifu Antony wa Padua na ile ya Bikira Maria zote hizo ni za enzi hizo.

Wakiwa wadogo mwanakwetu na wenzake wanakumbuka kuwa kulikuwa na watoto wa aina mbili wale walikwenda kusali wakiambatana na wazazi wao na wengine walikwenda kusali wenyewe. Maelekezo ya Mzee Ben watoto wote kanisani walipaswa kukaa mbele ya yale mabenchi ya kulia na upande wakushoto walikuwa wanakaa wanakwaya na watawa.

Wale watoto waliokuwa wakwenda kusali na wazazi wao wakiingia kanisa tu wazazi wao walitamani kukaa nao pamoja lakini Mzee Ben akawa anawaambia jamani hapa kanisa sisi wote ni watoto wa Mungu na kwenu wazazi mtambue hilo kuwa watoto wote wanapaswa kukaa mbele isipokuwa wale waliokuwa wadogo sana wanaobebwa tu.

Mara zote Mzee Ben alikuwa akisimama sehemu ya kuungamia huku akifuatilia misa hizo na wale wafanya vurugu na waliokuwa wakitokatoka nje ya kanisa kweli walichukuliwa hatua kali ikiwamo kufinywa na bakora.

Hilo lilikuwa linaleta tabu sana lakini mzee alikuwa mkali zaidi hata kuwafinya wale wakorofi waliendeleza utundu.

Pale Mbagala Misheni pana makaburi ya muda mrefu mno katika eneo ambalo lilikuwa wazi miaka mingi na eneo hili lilikuwa linavamia sana na watu wakajenga nyumba zao, Mzee Ben alikuwa mkali kwa wavamizi hao na kulilinda eneo hilo na mwanakwetu anakumbuka huyu Mzee Ben yeye mwenyewe akachangua eneo moja ambalo lilikuwa kando nyumba ndugu mmoja ambaye alikuwa akisumbua mno hili akifariki azikwe hapo.

Kweli baada ya muda Mzee Ben alifariki na kuzikwa hapo alipopachagua, lakini sasa eneo hilo halitumiki tena kuzikia wafu kwani limejaa.

Mwanakwetu kila anapokwenda Dar es Salaam huwa anajitahidi mno kusali kanisa hilo japokuwa sasa Mbagala si kijiji ni mji mkubwa, lakini wale watoto wa zamani rafiki wa mwanakwetu wamekuwa watu wazima.

Oktoba 2020, mwanakwetu alikutana na jamaa mmoja miongoni mwao akisimamia misa na kama kawaida yake mwanakwetu alimuuliza kaka huyu naona amerithi kazi ya Mzee Ben? Jamaa ilibidi acheke sana, akisema kuwa kweli sasa ni wakati wake wa kuwa mkali kama Mzee Ben kwa wale watoto wafanya vurugu kanisani ili waje kuwa na tabia njema kama yeye.

Maisha yaliendelea kama kawaida nayo Disemba 7, 2022 mwanakwetu alikwenda Dodoma Mjini kuwasalimia rafiki zake kadhaa waliokuwapo katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa alipofika hapo alikutana na rafiki zake kadhaa wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa ya Songwe, Tanga, Kigoma, Morogoro na Dar es Salaam alifanya nao mazungumo mengi akipata simulizi tele.

Hawa wajumbe wa Dar es Salaam mjumbe mmoja alikuwa miongoni mwa wale ambao alikuwa mtoto mtulivu aliyekuwa akikaa mbele kanisani na hakuwahi kuchapwa wala kufinywa na Mzee Ben wakati ule, huyu ni yule aliyeambiwa.“Kaka naona umerithi kazi ya Mzee Ben ? ” Oktoba 2022.

Mwanakwetu kama kawaida yake akasema, kijana wa Mzee Ben upo? Akajibu ndiyo akamwambia kaka bado unataka kumrithi Mzee Ben hadi Dodoma? Jamaa akacheka sana, akamuuliza mwanakwetu kwani Mzee Ben alikuwa chama chetu?.

“Unashangaa ! Wakati huo hapana na ndiyo maana yake ndiyo na hizo ni enzi za Katibu Mkuu wa CCM Rashidi Kawawa 1982-1990 na Horace Kolimba 1990-1995.”

Mrithi wa Mzee Ben aliuliza kwani Lawrence Gama alikaa kipindi gani ? Mwanakwetu alimjibu kuwa Gama alikuwa Katibu Mkuu wa CCM 1995-1997 yeye na Wilson Mukama walikatibu kipindi kifupi mno kati ya mwaka mmoja na miwili tu naye Mzee wetu Philip Mangula alikatibu kwa kipindi kirefu kuliko yoyote yule tangu 1997-2007.

Mwanakwetu akiwa hapo akamuombea kura William Lukuvi kwa ndugu yake huyu, jamaa akamjibu kuwa mheshimiwa hajawaona wajumbe hao na kuwaomba kura? Mwanakwetu akamwambia ndugu yake huyu kuwa kura zinaombwa kikaoni? Jamaa akacheka sana.

Mwanakwetu akauliza wagombea wengine wameshaomba kura? Mabasi yenu yalisimamishiwa wapi? Mrithi wa Mzee akacheka mno.

Mwanakwetu akaulizwa kwa nini anampigie debe mheshimiwa William Lukuvi wakati yeye ni mzee na huo ni muda wake kuwapisha vijana?.

Mwanakwetu akasema kuwa CCM ni chama cha wote na ana uhakika na uzoefu wa kiutendaji wa chama na serikali, hata ubunge wake jimboni kwake pia alipokuwa UVCCM hakudhulumu track suit za Chipukizi. Mwanakwetu alikaa nje ya ukumbi huo hadi matokeo yanatangazwa.

makwadeladius@gmail.com
0717649257

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news